Karibu Katika Blogu ya nafasi kwa Vijana


Blog hii inatoa taarfifa za nafasi kwa Vijana.Mmiliki wa Blogu hana uhisiano wa moja kwa moja na wahusika wa nafasi zilizotangazwa hapa

Search This Blog

Saturday, May 15, 2010

KESHO TUWASHE MISHUMAA YA KUMBUKUMBU-INTERNATIONAL AIDS CANDLELIGHT MEMORIAL

Tuwashe mishumaa kuwakumbuka wenzetu waliotangulia kutokana na AIDS
Nilikuwa nimejipumzisha nyumbani nikisikiliza matangazo ya redio katika kitua kimoja cha hapa Dar Es Salaam na ndipo nilipomsikia Dr. Isangula na Mama Mpendwa wakiongelea mada iliyonivuta kuongeza sauti ya redio yangu. Mada yenyewe ilihusu Tukio la Kimataifa la kuwasha mishumaa ya Kumbukumbu ya kuwakumbuka wenzetu waliotanguli mbele za haki kutokana na ugonjwa huu wa Ukimwi. Ugonjwa ambao umekuwa changamoto kubwa toka Bw. Clint Nyamryakunge alipoelezea dalili zisizoeleweka mwanzo wake kwa wagonjwa kadhaa huko mkoani Kagera mwaka 1983 ,ugonjwa ambao ulukuja kugundulika kuwa ni Ukimwi. Kwa sasa ugonjwa huu umeenea katika wilaya zote za 133 za Tanzania na takribani watu 200,000 hupata virusi vya ukimwi kila mwaka. Katika kipindi hiki cha Redio Dr. Isangula aliyejitambulisha kama Mratibu wa Shughuli za uwashaji mishumaa ya Kumbukumbu kwa nchi ya Tanzania aliyeteuliwa na Global Health Council, alisema, Tukio hili yaani ‘International AIDS Candlelight memorial event’ lilianza pia mwaka 1983katika jimbo la San Fransisco huo Marekani ,wakati ambao jamii za Mashoga zilikuwa zikiteketea kwa ugonjwa usiofahamika huku wataalamu wasijue mwanzo wake wala cha kufanya.Mashoga wanne Bobbi Campbell, Bobby Reynolds, Dan Turner na Mark Feldman kwa kujua kuwa watakufa ndani ya mwaka mmoja kwa ugonjwa huu wa ajabu bila msaada wowote wa kisiasa wakaamua kuelekeza macho yao katika ugonjwa kwa kuandaa maandamano mado kuanzia Castro District hadi City Hall San Fransisco wakiwa wamebeba mabango yalio andikwa ‘FOGHTING FOR OUR LIVES’ ,Maandamano ambayo yaliambatana na kuwasha mishumaa.
Toka Hapo Global Health Council ikaamua kusimamia tukio hili la kuwasha mishumaa na kwa sasa tukio hili limeeneza katika zaidi ya nchi 150 Ulimwenguni kote.
Mwamko wa Watanzania Ukoje?,Dr.Isangula anasema kwa Tanzania Candlelight ilianza mwaka 2003ambapo watu wachache tu waliandaa matukio madogo kuwakumbuka waliofariki kutokana na Ukimwi .Baadaye wadau mbalimbali kama Dr. Mayunga,Dr.Getruda Lwakatare,Tanzania AIDS Forum,Network of Women living with HIV(NETWO+),Save life Club, White Orange youth wamekuwa wakishiriki kuandaa tukio hili. Hata hivyo juhudi zinafanyika ili Candlelight memorial iweze kuingizwa katika mikakati ya kupambana na UKIMWI kitaifa.
Je Ushiriki wa TACAIDS,Wizara ya Afya au NACP Ukoje? Dr. Isangula anasema Amejaribu sana kuandika barua kwa TACAIDS,NACP na katibu mkuu wa wizara ya afya kuwaeleza kuhusu umuhimu wa candlelightili kuwakumbuka wenzetu waliofariki kwa ukimwi hasa akizingatia kuwa kama taifa limeweza kutenga siku maalumu kwa ajili ya Kumbukumbu ya Mwl Nyerere na Abeid Karume, kwa nini isitengwe siku maalumu ya kuwakumbuka maelfu wanaopoteza maisha yao kwa ukimwi japo kwa kuwawashia mishumaa?. Mwitikio wa viongozi ni mdogo lakini Dr.ISANGULA anamkumbuka na kumshukuru sana Dr.Fatma Mrisho,Mwenyekiti wa TACAIDS ambaye ameonyesha nia ya kuitambua Candlelight. Ni matarajio yetu kuwa nia hii sasa itaelekezwa kuwa vitendo kwa TACAIDS kuingiza Candlelight katika mipango mikakati yake.Tunashukuru kuwa baadhi ya mikoa kama Shinyanga tayari imeweka Candlelight katika mikakati yake.
Je wanaoishi na VVU Wanashirikishwa vipi?.Dr.ISANGULA anaamini mkuwa mtu yeyote mwenye VVU kama akipata huduma bora hawezi kufa kwa haraka,anatamani kuwa Watu waishio na VVU wapewe huduma bora kabisa ili kama wanakufa iwe ni kwa matatizo ya kawaida kama watu wengine na siyo kwa sababu ya Ukimwi. Hili litawezekana iwapo watashirikishwa katika kutengeneza sera na sheria zinazogusa huduma kwao. Miaka ya nyuma ilikuwa vigumu sana kuwaunganisha Wanaoishi na VVU katika kuandaa tukio hili,lakini wapo walioendelea kushiriki katika tukio hili pale lilipoandaliwa na wadau wengine.Lakini kwa miaka ya Karibuni tangu Tanzania AIDS Forum ianze kuandaa Candlelight ushiriki wa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi umekuwa mkubwa. Tunasheherekea ushiriki wa Baraza la Taifa la Watu Wanaoishi na VVU (NACOPHA) kupitia kwa NETWO+ wanashiriki kwa kiwango kikubwa sana mwaka huu . Wadau wengine kama,TANEPHA+,TNW+,NNEYOP+,NYP+,TAPOTI+,TAF Zinashiriki kwa aina moja au nyingine.Tunasheherekea uongozi mzuri wa Abinery Mpendwa,Mwenyekiti wa NETWO+ katika kuileta pamoja mitandao hii. Ni matarajio yetu kuwa ushiriki wa watu wanaoishi na VVU utaongezeka ili kutengeneza sauti ya Pamoja kudai haki zao.

Je tukio hili linafanyika lini? Tukio hili la uwashaji mishumaa ya kumbukumbu hufanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi wa tano kila mwaka.Mwaka huu litafanyika Jumapili ijayo ya Tarehe 16. Kauli mbiu ya Mwaka huu ni ‘More Lights for Human Rights’ ambayo imetafsiriwa kama Mwangaza zaidi kwa Haki za Binadamu’.Kauli hii inatokana na Kauli mbiu ya siku ya ukimwi duniani ya mwaka jana yaani ’Universal access & Human rights”.Kauli mbiu hii inawakilisha misingi mikuu ya utetezi kwa watu wanaoishi na VVU ambayo ni kuondoa unyanyapaa ,kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kujikinga na maambukizi,huduma bora za matibabu,na kuongeza fursa kwa watu waishio na VVU ili waweze kujitegemea na ushirikishwaji wao katika masuala muhimu yanayowagusa.

Je Kila Mtu anaweza Kuwasha mshumaa? Jibu ni ndiyo,kila mmoja anaguswa kwa aina moja au nyingine na Ugonjwa wa Ukimwi,kama unafanya Ngono bila kinga na hujapima afya yako uwezekano ni mkubwa kuwa una VVU.Kila mmoja amempoteza ndugu,rafiki,jirani,mfanyakazi mwenzake kwa ugonjwa huu. Ni vema tuwakumbuke wenzetu ili nasi tutakapokufa tukumbukwe kwa mishumaa. Ili kuonyesha upendo wapendwa wetu waliotangulia mbele za haki ni vema sasa tuweze kuwawashia mishumaa . Popote ulipo nyumbani,kazini,kanisani,msikitini unakaribishwa kuungana na mabilioni ya watu ulimwenguni kuwasha mishumaa ya kumbukumbu. Iwapo wapo watu wanawasha mishumaa katika vikundi ni vizuri ukahudhuria kwa kuwa sauti ya watu ni sauti ya Mungu ila ukishindwa waweza kuwasha mshumaa popote ulipo.

Kwa nini Tuwashe mishumaa? Mwanga wa Mshumaa una maana kubwa sana katika Candlelight. Mshumaa unajitolea kutoa mwanga kwa wengine pasipokujali kuwa wenyewe utaisha.Nasi tunahitaji kujitolea kuwasha mwanga wa Matumaini katika mioyo yetu na kuweka ahadi za mapambano dhini ya maambukizi ya VVU.Siku hii ya kuwakumbuka wenzetu waliotangulia mbele za haki ni siku nzuri ya kutafakari wajibu wa kila mmoja katika kuzuia maambukizi ili idadi ya tunaowakumbuka kila mwaka ipungue. Tuwashe mishumaa itumulike mioyoni mwetu,tuweke ahadi ya kuzuia maambukizi zaidi.Kwa watu ambao uwashaji wa mishumaa unakinzana na imani yao,hata mwanga wa tochi unakubalika.

Ni matumaini yangu kuwa watu wote tutajumuika katika kuwasha mishumaa jumapili hii ili kuwakumbuka wenzetu waliotangulia na kuweka ahadi mioyoni mwetu ya kupambana na maambukizi zaidi.

tembelea www.candlelightmemorial.org au tuma e mail kwa kaisa079@yahoo.com kwa taarifa zaidi

No comments:

Post a Comment