Karibu Katika Blogu ya nafasi kwa Vijana


Blog hii inatoa taarfifa za nafasi kwa Vijana.Mmiliki wa Blogu hana uhisiano wa moja kwa moja na wahusika wa nafasi zilizotangazwa hapa

Search This Blog

Saturday, May 15, 2010

HOTUBA YA VIONGOZI KWA AJILI YA UWASHAJI MISHUMAA KESHO JUMAPILI

YIFUATAYO NI HOTUBA YA WAGENI RASMI
May 16th 2010
Nianze kwa kusema, Sote tunatambua kuwa UKIMWI ni moja wapo ya Changamoto kubwa sana Duniani kote.Karibu kwa robo karne sasa ugonjwa huu umekuwa ukiathiri jamii nyingi sana Katika ngazi ya kitaifa,familia,kiuchumi na watu mamilioni wamepoteza maisha yao.Hadi sasa bado wanajamii tunaamini kuwa tunaweza kutatua janga hili na Kupunguza maambukizi mapya .
Ugonjwa ambao umekuwa changamoto kubwa toka Bw. Clint Nyamryakunge alipoelezea dalili zisizoeleweka mwanzo wake kwa wagonjwa kadhaa huko mkoani Kagera mwaka 1983 .Kwa sasa ugonjwa huu umeenea katika wilaya zote za 133 za Tanzania na takribani watu 200,000 hupata virusi vya ukimwi kila mwaka.
Tukio hili yaani ‘International AIDS Candlelight memorial event’ lilianza pia mwaka 1983 katika jimbo la San Fransisco huo Marekani na leo hii nchi zaidi ya 110 duniani lo hiizinawasha mishumaa ya kumbukumbu.
Tukio hili la uwashaji mishumaa ya kumbukumbu hufanyika kila Jumapili ya tatu ya mwezi wa tano kila mwaka.Mwaka huu litafanyika Jumapili ya leo ya Tarehe 16.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ni ‘More Lights for Human Rights’ ambayo imetafsiriwa kama ‘Mwangaza zaidi kwa Haki za Binadamu’. Kauli hii inatokana na Kauli mbiu ya siku ya ukimwi duniani ya mwaka jana yaani ’Universal access & Human rights”.Kauli mbiu hii inawakilisha misingi mikuu ya utetezi kwa watu wanaoishi na VVU ambayo ni kuondoa unyanyapaa ,kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za kujikinga na maambukizi,huduma bora za matibabu,na kuongeza fursa kwa watu waishio na VVU ili waweze kujitegemea na ushirikishwaji wao katika masuala muhimu yanayowagusa.

Kwa kutoa heshima zetu na kuwakumbuka ndugu,Marafiki ,majirani zetu na wanajamii wenzetu kwa ujumla ambao wamepoteza maisha yao kutokana na Gonjwa hili, tunapata nafasi pia kuunga mkono Mapambano ,kushirikiana na kuwasaidia wenzetu wanaoishi na VVU na pia tunaelimishana na kukumbushana wajibu wetu wa kujilinda na kuwalinda wote ambao hawajaambukiza VVU.

Kila mwanjamii anao wajibu wakujinga na kumkinga mwenzake asipate maambukizi ya VVU. Wajibu wa wetu ni kuhakikisha tatizo hili la VVU/UKIMWI linaisha kabisa,lakini hatuwezi kufanikisha hili kama kila mtu atapambana peke yake na hata imani pekee kuwa tatizo hili litaisha haitoshi.Ni lazima sasa tuchukue hatua za Pamoja kuanzia Katika ngazi ya jamii na serikali ni lazima tushirikiane kupambana.Na kuwepo kwangu hapa leo ni dalili ya Ushirikiano Katika Mapambano .
Napenda kuwapongeza Ebeneza Group,Fmily Health Internatioal,YADEC na wadau wote ambao wamefanikisha tukio hili leo.N i lazima kila mmoja wetu leo aweke Azimio la Kupambana na UKIMWI kwa pamoja,tena kwa nia ya dhati kabisa .Ni lazima tupaze sauti zetu kwa pamoja,kwa kuwa sauti ya wengi ni sauti ya Mungu,tupaze sauti kwa Viongozi wa serikali Katika ngazi ya kijiji, Kata,Wilaya ,Mikoa,kitaifa na kimataifa ili waongeze bajeti kwa ajili ya Mapambano ya VVU/UKIMWI .Tupaze sauti kwa wale wanaopata misaada kwa ajili ya Mapambano waitumie kwa matumizi sahihi.Tupaze sauti kwa viongozi wetu wa kijamii ili wawe mfano wakuigwa Katika jamii kwa kuhimiza Mapambano,ili waweze kutoa huduma zaidi kwa Waishio na VVU ,Kuwashirikisha Katika kuandaa programu za kitaifa zinazohusu Mapambano.Kupaza sauti kwa wafanya biashara kutoa sehemu ya faida yao Katika mapambano,kwani iwapo watu wote watapata VVU/UKIMWI hakuna atakayenunua bidhaa zao.Kupaza sauti kwa vyombo vya habari kutoa nafasi zaidi kwa habari zinazohusu Mapambano. Kupaza sauti kwa wenye fedha na nafasi kubwa ya kijamii kuacha kutumia vyeo,kazi na fedha zao kufanya ngono zembe na hatimaye kuchangia kuendeleza maambukizi.
Sera zetu za kupambana na VVU/UKIMWI ni lazima ziwe na usawa na zizingatie hali halisi.Tiba kwa magonjwa nyemelezi lazima pia iendane na uhamasishaji mkubwa wa kuzuia maambukizi Katika ngazi zote na lazima uhamasishaji huu uzingatie Haki za binadamu .Mapambano yetu pia ni lazima yatilie maanani Uhusiano kati ya UKIMWI na Kifua Kikuu,Malaria na Matatizo mengine.
Ni lazima tuondokane na woga wa kushirikiana na wenzetu waishio na VVU/UKIMWI,ni lazima tuache unyanyapaa na kuwatenga,natoa wito kwa wanjamii kutambua kuwa njia kuu kabisa ya maambukizi ni ngono isiyo salama,japo njia nyingine kama vile maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa ujauzito,kuchangia vitu vinavyotoboa ngozi n.k ni vema zizingatiwe,lakini kiasi kikubwa cha maambukizi kinatokana na ngono isiyo salama,ni vema sasa wazazi wakawa wawazi kwa watoto wao kuongea nao masuala yanayohusu mahusiano ya kimapenzi.Sote kwa pamoja tunaweza kulizuia janga hili.Kila mmoja na awe mwalimu wa kuelimisha wenzake,kila mmoja awe balozi wa kuwaelekeza wenzake,kila mmoja awe askari wa kuwalinda wenzake dhidi ya HIV/AIDS na kila mmoja awe Ngao ya kujilinda mwenyewe.
Kwa hivi tulivyokusanyika leo kuwakumbuka wenzetu,tunawasha mwanga wa mshumaa mioyoni mwetu ,mwanga wake umulike juhudi zetu ili tutafute ufumbuzi wa pamoja ili kulimaliza tatizo hili la HIV/AIDS
ASANTENI SANA

No comments:

Post a Comment